Uongozi wa klabu ya Yanga umethibitisha kuwasili kwa uongozi wa Pyramids na leo asubuhi watawasili jijini mwanza kwa ajili ya maandalizi ya mahala pa kufikia timu hiyo.
Makamu mwenyekiti wa Yanga amethibitisha kuwasili kwa maofisa watatu wa Pyramids kwa ajili ya maandalizi ya mahali timu hiyo itakapoweka Kambi.
Mwakalebela amesema maofisa hao waliwasili jijini Dar es Salaam alfajili ya tarehe ya tarehe 23 Oktoba na baadaye kuelekea jijini Mwanza kukamilisha maandalizi yao.
Mwakalebela ameongeza kuwa msafara kamili wa timu hiyo utawasili leo tarehe 24 Oktoba saa moja jioni kwa ndege maalumu itakayotua jijini Mwanza na utafikia hoteli ya Malaika.
Tangu kuanza kwa mwezi Oktoba klabu ya Pyramids imecheza michezo 4 na imeshinda michezo 2 na sare 2, klabu hiyo imefunga mabao 7 na kufungwa mabao 5 kwenye mechi nne ilizocheza.
0 Comments