Yanga wao wameendelea kuvutana mashati kuhusu hatma ya Kocha Zahera na baadhi wameanzisha kampeni za kutaka Mkongo huyo awaachie timu yao.
Wakati hayo yakitokea Klabu ya Pyramids imeendelea kujiweka sawa na mchezo huo na inaonyesha hali ya ushindani kwenye michuano hiyo.
Klabu hiyo imecheza michezo 5 ya ligi kuu Misri na kushinda michezo 3 ikitoka sare 2 na kuwa na pointi 11 ikiongoza msimamo wa ligi kuu Misri.
Yanga inapaswa kushinda mabao kuanzia 2-0 au 3-1 ili kuweza kuingia moja kwa moja hatua za makundi kombe la Shirikisho.
0 Comments