advertise with us

ADVERTISE HERE

OLE GUNNAR KUTIMULIWA MANCHESTER UNITED HIVI KARIBUNI

Unaweza kusema Manchester United imekwisha au ndio zama za ufalme wao zilimalizika mwaka 2013 chini ya Ferguson.


Kocha wa sasa Ole Gunnar ameendelea kukalia kuti kavu baada ya kupata pointi 9 tu kati ya michezo 8 Manchester United waliyocheza ligi kuu Uingereza.

Manchester imekuwa na msimu mbaya zaidi baada ya kufanya hivyo miaka ya 1980 na sasa hali hiyo imeingia klabuni hapo huku lawama zote zikimwangukia kocha wa timu hiyo.

Manchester United imecheza mechi Tano hivi karibuni huku ikishinda mechi moja tu tena kwa ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Leicester city, Mechi nyingine ni dhidi ya Arsenal 1-1 ,AZ 0-0 na ikipoteza bao  1-0 toka kwa Leicester.

Matokeo hayo yanaipeleka Manchester United katka nafasi ya 12 huku ikiteremka kwa nafasi 2 toka 10 wiki iliyopita.

Wiki ijayo timu hiyo itapambana na Liverpool timu ngumu na nzuri zaidi msimu huu kwa kushinda mechi zote 8 ikifunga mabao20 na kuruhusu 6 tu .

Hatma ya Ole Gunnar itaamuliwa baada ya mchezo huo na ni wazi anaweza timuliwa wakati wowote kuanzia sasa.

Post a Comment

0 Comments