advertise with us

ADVERTISE HERE

NGORONGORO HEROES WAWASILI DAR, MBAPPE AWA GUMZO

Hatimae kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 kimerejea nchini kwa shangwe baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa CECAFA U-20 michuano iliyofanyika nchini Kenya.


Ngorongoro Heroes iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wa mashindano hayo. Kivutio katika mapokezi hayo alikuwa ni mchezaji mahili kabisa Kelvin John "Mbappe" aliyeiongoza timu hiyo kutwaa kombe hilo kwa kufunga mabao 7 hivyo kutwaa kiatu cha ufungaji bora.

Mbappe hakuishia hapo kwani ndiye mchezaji aliyecheza kwa kiwango cha juu na kupelekea kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa michuano hiyo.

Hivi karibuni mchezaji huyo alielekea nchini Ubelgiji kufanya majaribio katika klabu ya KR Genk anayoichezea Mbwana Samatta na kama mambo yatakwenda vyema basi mchezaji huyo ataichezea timu ya vijana ya KR Genk.

Post a Comment

0 Comments