BETI NASI UTAJIRIKE

MSAFARA WA NDANDA WAPATA AJALI UKIELEKEA KAGERA

Msafara wa wachezaji wa Ndanda FC umepata masaibu baada ya timu hiyo kupata ajali ikielekea mkoani Kagera kuwakabili Kagera Sugar mchezo wa Ligi kuu Vodacom. 



Chanzo cha ajali hiyo ni utelezi kutokana na mvua kubwa. katika ajali hiyo wachezaji waliopata majeraha ni Aziz Sibo, Paul Mahona, Hemed Koja, Nassoro Saleh, Omar Ramadhan. 

Msemaji wa klabu hiyo alisema Idrisa Bandali "Utelezi umechangia maana imenyesha mvua kubwa, Kuna gari ilisimama ghafla kwa mbele dereva wetu akawa anajaribu kufunga breki ikafeli na kuigonga basi ya Mtei kwa nyuma, sasa hivi majeruhi wapo Hospitali ya Wilaya Nzega, ilipotokea ajali sio mbali na Nzega Mjini kwahiyo unafanyika utaratibu wa usafiri ili kikosi kifike Nzega Mjini, gari haijaanguka ila imeumia sana upande wa dereva na haiwezi kumudu tena safari"

Wachezaji wote walipelekwa hospitali kwa vipimo zaidi huku taarifa kamili kutoka TFF kungojewa kama mchezo huo umeahirishwa au utapigwa vivyo hivyo.

Wachezaji hao walipata ajali hiyo na basi la timu hiyo lenye namba za usajili T 514 DBU aina ya Toyota Coaster.

Mtandao wa Amospoti.com unawapa pole viongozi na wachezaji wa timu ya Ndanda na tupo nyuma yenu kipindi hiki kigumu.

Post a Comment

0 Comments