advertise with us

ADVERTISE HERE

MOURINHO AMKUBALI RONALDO ZAIDI YA LIONEL MESSI ,CRISTIANO

Kocha wa zamani wa Manchester United ameibua hoja kwa wadau wa soka baada ya kuulizwa ni yupi mchezaji bora wa dunia kisha kuwakacha Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.


Mourinho amesema mchezaji bora kwa upande wake ni Ronaldo De Lima na si Cristiano Ronaldo wala Lionel Messi.

Mourinho alikuwa kocha msaidizi wa Barcelona msimu wa 1996/97 chini ya kocha BobRobson na wakati huo alishuhudia Ronaldo akifunga mabao 47 kwenye mechi 49 za mashindano mbalimbali.


Baadaye Ronaldo alielekea Intermilan,Real Madrid na aliisaiia Brazil kutwaa kombe la dunia mwaka 2002 kisha kustaafu mwaka 2011.

Mourinho amemfundisha Criatiano Ronaldo kwa miaka mitatu akiwa Real Madrid na kuuangalia Lionel Messi kwa kipindi chote cha uchezaji. Wachezaji hawa wanatajwa kuwa bora zadi kwa kipind cha miaka 15.

Mourinho amesisitiz hakuna mchezaji anaeweza kufikia uwezo wa Ronaldo de lima na amewazidi Messi na Cristiano sema majeraha yamepelekea kuharibu kipaji chake.

"Nilipokuwa Barcelona na Bob Robson niligundua De lima ni mchezaji wa kipekee niliyepata kumuona. kwa umri wa miaka 19 alifanya mambo mengi makubwa mwaka 1997 Barcelona ilichea dhidi ya PSG mjini Rotterdam na Ronaldo alifunga goli mno lililoipa Barcelona ushindi wa bao 1-0"

Post a Comment

0 Comments