advertise with us

ADVERTISE HERE

MORINGA NI MWIBA MKALI AWATUMIA SALAMU SIMBA

Mshambuliaji mpya wa Yanga aliesajiliwa hivi karibuni DAVID MORINGA ameibua hisia tofauti kwa wapenzi wa Yanga baada ya leo hii kudhibitisha ubora wake dhidi ya Polisi Tanzania


Moringa alionekana si chochote kwenye mchezo wake wa kwanza dhidi ya Ruvu shooting mchezo ambao Yanga ilipoteza kwa bao moja bila.

Mashabiki wa Simba walianza kumbeza Moringa kwa kushindwa kufunga mechi za majaribio na kudhani mwili wake si chochote na mzito kwenye kufunga.

Kwenye mchezo wa jana dhidi ya Polisi Tanzania aliwafunga mdomo Simba kwa kufunga magoli mawili muhimu yaliyopelekea droo ya mabao 3-3.

Moringa alipiga kichwa kizito kilichomshinda kipa wa Polisi Tanzania alieingia na mpira golini . Goli la pili Moringa alipewa faulo nje ya 18 na alipiga shuti kali lililoingia golini moja kwa moja.

Kwa magoli hayo Moringa anaanza kufukuza kiatu cha dhahabu kimya kimya nyuma ya Kagere aliecheza mechi 4 na kuwa na magoli 6.

Post a Comment

0 Comments