Mwenyekiti wa Makampuni ya Mohamed Enterprises Tanzania Limited ameendelea kuwashukuru wadau mbalimbali kwa kuonyesha upendo kipindi alipokuwa ametekwa na wasiojulikana.
Mo Dewji ametimiza mwaka mmoja tangu alipotekwa na kuachiliwa huku kukiwa hakuna sababu yoyote iliyoelezwa nini hasa chanzo cha kutekwa kwake.
Kupitia mitandao ya kijamii ameandika:
"Hali niliyopitia ilionyesha nguvu ya mitandao ya kijamii iliyopelekea umma kushinikiza niachiwe nikiwa salama. Asanteni malaika wote ambao mlionyesha upendo wa kweli na kunijali kupitia post / hashtag mlizoandika. Hii ilinishangaza sana. Nina deni kwenu milele. Daima Mungu awe nanyi nyote 🙏🏽
//
The power collective action through social media to create public pressure for my wellbeing and safe release was unimaginable. Thank you to all the angels on keyboards who showed genuine love and care for me through their posts / hashtags. This truly blew me away
0 Comments