Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara klabu ya Simba SC inaweza kuwa wafungia wachezaji wake wanne kwa makosa mbalimbali likiwemo la utovu wa nidhamu.
Wachezaji hao ni Gadiel Michael, Chama ,Nyoni n Jonas Mkude. Wcezaji hao wanakabiliwa na kosa la kutohudhulia michezo miwili iliyopigwa kanda ya ziwa ukiwemo ule wa Kagera Sugar vs Sugar na ule wa Biashara UNITED vs Simba.
Mbali na kukosekana wachezaji haowanaounda kikosi ca kwanza timu hiyo ilishinda mechi zote mbili na kurejea Dar es Salaam kwa michezo inayofuata. Mchezaji Jonas mkude anatuhumiwa kutoroka kambini siku moja kabla ya safari huku wachezaji hao wengine wakishutumiwa kwa makosa ya kuto safiri na timu hiyo.
Kwenye barua iliyotolewa uongozi wa timu hiyo umekanusha habari zilizosambazwa na vyombo mbalimbali vya habari juu ya kufungia wachezaji hao kwa kipindi cha mwezi mmoja. Aidha uongozi umesema umeunda kamati maarumu kuchunguza tukio hilo na utatoa shauri baada ya wachezaji wa timu hiyo kurejea kutoka kwenye timu zao za taifa.
0 Comments