Kocha wa Argentina amesisitiza Messi atarejea mwezi Novemba kuitumikia timu yake ya taifa Argentina
Messi alifungiwa mechi tatu na shirikisho la soka Amerika Kusini CONMEBOL kwa kugoma kuvaa medali na kusema shirikisho hilo lilipokea rushwa toka kwa Brazil.
Messi alianza kulituhumu shirikisho hilo baada ya kufungwa mabao 3-1 na wenyeji wa mashindano hayo Brazil na baadaye kuifunga Chile kisha kutwaa nafasi ya tatu ya michuano hiyo na Brazil ikinyanyua kombe hilo.
CONMEBOL ilimfungia Messi na adhabu yake itahitimika mwezi Novemba kisha nahodha huyo kurejea kikosi cha Argentina.
Mbali na Messi kukosekana kwenye mchezo uliochezwa hapo jana dhidi ya Equador timu ya taifa Argentina iliibuka na ushindi wa mabao 6-1.
0 Comments