advertise with us

ADVERTISE HERE

MESSI AREJEA UWANJANI , WAWILI WALA KADI NYEKUNDU BARCELONA IKISHINDA 4-0

Mchezaji bora wa kiume tuzo za FIFA  Lionel Messi amerejea rasmi uwanjani baada ya kukosekana kwa mechi kadhaa ligi kuu Hispania.

Mchezaji huyo amerejesha makali yake ya kufumania nyavu baada ya kufunga  bao 1 kati ya manne  waliyoshinda dhidi ya timu ngumu ya Seville.

Nyota wa timu hiyo Louis Suarez alikuwa wa kwanza kupachika bao dakika ya 27 akifuatiwa na Arturo Vidal dakika ya 32, Dembele  dakika ya 35 na mfalme wa klabu hiyo Lionel Messi dakika ya 78.

Kituko cha mchezo huo ni kutolewa kwa kadi mbili nyekundu kwa wachezaji wawili wa ttimu hiyo  Anold Araujo na Dembele . Anold alitokea benchi na hakumaliza mchezo huo kwani alitolewa nje dakika ya 87.

Matokeo hayo yanaifanya Barcelona kushikiria nafasi ya nyuma ya wapinzani wao wakubwa Real Madrid wenye pointi 18 na Barcelona pointi 16.

Tarehe 26/10 timu hizo zitakutana kwa mara ya kwanza msimu huu na atakaeshinda atajiwekea nafasi nzuri ya kuongoza ligi mpaka mzunguko wa pili wa ligi.

Post a Comment

0 Comments