Mchezaji wa Klabu ya Yanga Kalengo atalazika kukaa nje ya uwanja mpaka mwaka 2020 baada ya kuvunjika eneo lake la mguu wakati akiitumikia klabu yake kwenye mchezo wa kirafiki na Pamba
Uongozi wa Yanga umethibitisha kuumia kwa mchezaji huyo. Asubuhi ya leo Oktoba 23 Yanga ilicheza mchezo wa kujiimarisha dhidi ya Pamba FC ya Mwanza mchezo uliomalizika kwa Yanga kushinda mabao 2-1.Kwenye mchezo huo Yanga iliwatumia wachezaji ambao hawakucheza dhidi ya Mbao hapo jana huku Kalengo akiwa ni mmoja wao. Kuumia kwa mchezaji huyo ni pigo kwa Yanga na inaaminika atakaa nje ya uwanja kwa wiki nane hadi kumi na mbili.
Uongozi wa Yanga umethibitisha kumsafirisha nyota huyo mpaka jijini Dar es Salaam kwa ajili ya vipimo na matibabu sahihi.
Yanga ipo jijini Mwanza ikijiandaa na mechi ya kombe la shirikisho dhidi ya Pyramids ya nchini Misri mchezo utakaopigwa tarehe 27 Oktoba jijini humo.
0 Comments