Mshambuliaji kinda wa klbu ya PSG na Ufaransa pamoja na Raheem Stering wa Manchester City na Uingereza wameonekana tishio zaidi hapo jana kwa kuweka rekodi ligi ya mabingwa Ulaya.
Wachezaji hao waliingia uwanjani kutetea timu zao kwenye ligi ya mabingwa Ulaya. Sterling alikuwa ndani ya uzi wa Manchester City dhidi ya Atlanta. Mchezo huo uliopigwa dimba la ETIHAD ulimalizika kwa Manchester City kushinda mabao 5-1 huku Sterling akiibuka nyota wa mchezo kwa kufunga mabao 3 na Aguero akifunga mawili. Matokeo hayo yameifanya Manchester City kuongoza kundi C ikiwa na pointi 9 kwenye michezo mitatu.
Kwa upande wa PSG wao walikaribishwa na CLUB BRUGGE kwenye mchezo wa kundi A. Mchezo uliomalizka kwa PSG kushinda mabao 5-0 huku kinda wa timu hiyo Kylian mbappe akiibuka nyota wa mchezo kwa kufunga mabao matatu na Di Maria akifunga mawili.
WAWEKA REKODI MPYA
Sterling na Mbappe wameweka rekodi mpya usiku wa tarehe 23-10-2019
1.wamefunga Hat trick zao za kwanza msimu huu,
2.Hat trick hizo zote zimefungwa kipindi cha pili
3.wamezisaidia timu zao kushinda mabao matano kila mmoja
4. Aguero(Manchester City) amefunga mawili na Icardi (PSG)akifunga mabao mawili.
5.Aguero na Icardi wote wanachezea timu ya taifa Argentina hivyo kuwafanya wachezaji hao kuwa na rekodi nzuri wakiwa na wachezaji hao wa Amerika ya Kusini.
0 Comments