advertise with us

ADVERTISE HERE

MANCHESTER UNITED NA ARSENAL WASAHAU LIGI YA MABINGWA ULAYA.

Baada ya kuungoja kwa hamu mchezo wa ligi kuu Uingereza kati ya Manchester United dhidi ya Arsenal hatimae timu hizo ziliumana kwenye dimba la Old Trafford na matokeo yake yalikuwa ni kero kwa kila mpenzi wa soka.

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku  Manchester United wakiutawala mchezo , dakika ya 43 Kiungo kinda wa klabu hiyo Mc Tominay alipiga shuti lililozaa bao la kuongoza na mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Manchester United ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili timu hizo zilirejea dimbani na dakika ya 59 Arsenal walipata bao la kusawazisha kupitia kwa Pierre Aubameyang na mpaka filimbi ya mwisho timu hizo zilifungana bao 1-1.

Kwa mtazamo wa kimchezo timu hizo zimeonekana kuanza msimu huu vibaya na hazionyeshi kuleta ushindani kwa Manchester City wala Liverpool.

Timu hizo zimecheza jumla ya michezo 7 na zimeshinda michezo 2 huku zikidroo 3 zimejikuta zikijikusanyia pointi 9 tu katika michezo 7.

Nini maana ya  matokeo haya 
Kama timu hizo zitaendelea kucheza namna hiyo basi nina uhakika zitapata wakati mgumu kucheza hata Europa msimu ujao.

Tatizo ni nini ?
Timu hizo zinaonekana kukosa washambuliaji wa uhakika hasa kwa Manchester United ambayo humtegemea Rashford ,mwenye kiwango kibaya msimu huu na amekuwa akikosa nafasi za wazi.
Kwa upande wa Arsenal wao wanamtegemea Pierre Aubameyang lakini mchezaji huyo anapaswa kuwa na viungo wa kueleweka ili watengeneza pasi zaidi.

Nini kinafuata
Timu hizo zitakuwa na michezo ya Europa ligi siku ya Alhamisi Arsenal ikiikaribisha Standard Liege na Manchester United ikiifuata Eredivisie outfit AZ. Kwa Upande wa ligi kuu Uingereza. Manchester itaikaribisha New Castle United huku Arsenal ikiikaribisha Bournemouth 



Post a Comment

0 Comments