Manara amejipanga kuwapokea wachezaji hao mara tu watakapotua jijini Mwanza na kuwapa sapoti ya nguvu siku ya mechi dhidi ya Yanga. Msemaji huyo amekuwa na ugomvi na mashabiki wa Yanga kwani wamekuwa wakizipa sapoti timu za kigeni kwenye michezo ya Simba kimataifa.
Tangu ratiba ya mechi hiyo itoke Manara amekuwa akirusha vijembe kwa Yanga na amesema timu hiyo haiwezi kufanya lolote dhidi ya Pyramids . Yanga imeonekana kuwa dhaifu msimu huu baada ya kucheza mechi 4 za ligi ikikusanya pointi 7 na kufunga mabao 7, Wapinzani wao Simba wameheza mechi 5 wakipata pointi 15 na kumfanya Manara awe kifua mbele wakati wote
Manara amesisitiza kuondoka leo asubuhi kuelekea jijini Mwanza akiwa na timu hiyo na aliandika hivi
"Msiyemtaka kaja,Na Insha'Allah kesho ntaongozana nao mchana kwenda Mwanza,mm nikienda ktk Graduation ya Bwiru Sec,Naomba wanafunzi wa Bwiru mje kunifuata Airport saa saba adhuhuri!!
Muhimu team Pyramids tujuane mapemaaaaaaa"
0 Comments