advertise with us

ADVERTISE HERE

MAJERAHA YA NEYMAR KUMUWEKA NJE WIKI NNE

Mshambuliaji wa timu ya taifa Brazil na Klabu ya PSG hatakuwepo ndani ya uwanja kwa kipindi cha wiki nne kutokana na majeraha aliyoyapata jumamosi iliyopita akiitumikia Brazil.


Dakika ya 12 kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Brazil dhidi ya Nigeria uliopigwa huko Singapore na kumalizika kwa sare ya mabao 1-1.

Daktari wa klabu ya PSG amedhubitisha mchezaji huyo kupata majeraha mguu wake wa kushoto eneo la kifundo hivyo atapaswa kukaa nje ya uwanja kwa wiki 4 mpaka tarehe 11 mwezi novemba.

Neymar atakosa mihezo miwili mmoja n ligue 1 dhidi ya Marseile na mwingine ni ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Brugge.

Msimu huu Neymar ameanza vizuri ligi kuu nchini ufaransa Ligue 1 akifunga mabao 4 kati ya mechi 5.


Post a Comment

0 Comments