Magori alipotembelea ofisi za Mo Dewji
Kabla ya uteuzi huo Bw. Magori alikuwa ameachia ngazi ya Uongozi wa mabadiliko kwa klabu ya Simba kutoka kuwa timu ya wanachama na kuifanya kuwa timu yenye kupokea wawekezaji.
Kwa usimamizi mzuri wa Magori klabu hiyo ilifanikisha mchakato huo na Mohammed Dewji alipata asilimia 49 ya hisa za Simba huku asilimia 51 zikibaki kwa wanachama wa Simba.
Mohammed Dewji ameamua kulipa fadhira kwa kumteua Bw.Magori kama mshauri binafsi hasa kiutendaji kwenye klabu ya Simba.
Barua ya wazi kutoka kwa Mohammed Dewji kwenda kwa Bw. Magori
Mo Dewji alithibitisha taarifa hiyo kwa kuichapisha kupitia kupitia kurasa zake za mitandaoni Mo Dewji aliandika hivi "Napenda kutangaza rasmi kuwa nimemteua Ndg. Crescentius Magori kuwa mshauri wangu binafsi kama Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba. Anauzoefu mkubwa wa soka la Afrika na ninaamini uwepo wake utaongeza nguvu kwenye safari yetu ya kuifanya Simba kuwa moja ya klabu yenye mafanikio makubwa zaidi barani Afrika."
Mtandao wa www.amospoti.com unampongeza Bwana Crescentius Magori kwa uteuzi huo na kumtakia mafanikio mema katika kuijenga klabu ya Simba.
0 Comments