Mabingwa watetezi wa ligi ya mabingwa Ulaya wameendelea kupata matokeo kwa tabu mno kulinganisha na wanavyofanya ligi kuu nchini Uingereza.
Liverpool iliikaribisha Anfield timu ya Red Bull na mpira ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu.
Dakika 9 ya mchezo Liverpool walijipatia goli la kuongoza kupitia Sadio Mane. Andrew Robertson alipachika bao la pili dakika ya 25 na Mo Salah akifunga bao la tatu dakika ya 36 na Chan kutafuta bao la kufutia machozi dakika ya 39, mpaka timu hizo zinakwenda mapumziko Liverpool ilikuwa ikiongoza kwa mabao 3-1.
Kipindi cha pili Red Bull walirejea mchezoni kupitia mchezaji wake Minamino aliepachika goli la pili dakika ya 56 na goli la tatu lilifungwa na Halland dakika ya 60. Mpaka hapo matokeo yalikuwa ni 3-3 kabla ya Mo salah kufunga bao la 4 dakika ya 69.
Kwanini nasema Liverpool hawaendi kokote
Wakiwa ugenini dhidi ya Napoli kwenye mchezo wa kwanza ligi ya mabingwa ulaya walipoteza mchezop huo kwa mabao 2-0. mbali na hayo kwa michezo miwili ameruhusu magoli matano kufungwa. Kama atakutana na timu ngumu kwenye hatua zinazofuata basi atalazimika kutumia nguvu zaidi kushinda.
0 Comments