klabu ya Yanga imeshusha viingilio vya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids FC utakaopigwa Jumapili ya wiki hii katika Uwanja wa CCM
Kirumba, jijini Mwanza.
Maamuzi hayo yametokana na mashabiki wa timu hiyo mkoani Mwanza kuomba viingilio hivyo vishuhswe ili kutoa urahisi wa wingi kujitokeza uwanjani.
Kwa sababu hiyo, uongozi umeridhia ambapo hivyo sasa viingilio vitakuwa: mzunguko, 7,000/= badala ya 10000 ya mwanzo huku VIP itakuwa 20,000/= na Royal, 50,000.
Kupunguzwa kwa viingilio hivyo kunaweza kukawa kumeleta msala kwa namna moja ama mwingine kwa wapinzani wao Pyramids kutokana na wingi wa mashabiki watakaoingia uwanjani.
Kupunguzwa kwa viingilio hivyo kumepokelewa kwa wingi na mashabiki pamoja na wanachama wa Yanga mkoani Mwanza, kinachotarajiwa hivi sasa ni kuijaza kwa wingi CCM Kirumba ili kuwazomea waarabu.
0 Comments