Kocha waYanga, Mwinyi Zahera.
Kauli ya Zahera imekuja kufuatia kutofanya mabadiliko baada ya kuweka wazi kuwa wachezaji wake walikuwa kwenye mipango yake.Zahera alisema alichelewesha kufanya mabadiliko akiamini mechi ingemalizika kwa sare ya 1-1 na wangeweze kufikia hatua ya kupiga matuta.
Lakini Zahera ameibuka na kusema kama angefanya mabadiliko mapema haswa kuwatoa Abdulaziz Makame na Feisal Salum 'Toto' ambao aliona wamechoka, matokeo yangekuwa mengine.
Fei Toto
"Kama ningefanya mabadiliko mapema ya Toto na Makame waliokuwa wamechoka katika safu ya kiungo ya timu yangu, matokeo yasingekuwa hivyo."Nipende tu kuwapongeza wachezaji wangu kwa kupambana vizuri na sasa tunaelekeza nguvu zetu zote kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho."
0 Comments