Mara baada ya kutua uwanja wa KIA uongozi na wachezaji walielekea hotelini na ilipofika saa 4:00 timu hiiyo ilielekea uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa ajili ya mazoezi ya mwisho ndipo wakakutana na kizaa zaa cha FIESTA.
Kocha wa klabu hiyo Patrick Aussems aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instagram na kushangazwa na majukwaa ya Fiesta yakiendelea kujengwa ili hali wao wanamchezo tarehe 27 Oktoba.
Timu hiyo imeshindwa kufanya mazoezi uwanjani hapo kutokana na uwanja huo kuanza kujaza mashabiki mbali mballi waliohudhulia tamasha hilo.
Tamasha hilo limefanyika usiku na mara tu baada ya tamasha hilo kumalizika basi majukwaa yote yataondolea na Simba itajiandaa kuwakabili wapinzani wao Singida United.
0 Comments