BETI NASI UTAJIRIKE

KIBOKO WA YANGA,SIMBA ANG'OKA BODI YA LIGI AKABIDHIWA NAFASI MPYA TFF

Nafasi ya mtendaji mkuu bodi ya ligi (TPBL) iko wazi baada ya kumaliza muda wake Boniface Wambura. Katibu mkuu wa shirikisho la soka Tanzania (TFF). Bw.Wilfred Kidao



alisema mchakato wa kumtafuta mrithi wa Wambura umeanza na Wambura amepewa nafasi nyingine ndani ya Shirikisho hilo.

Wambura atakuwa mkurugenzi wa idara ya Habari na masoko ndani ya TFF ambayo itakuwa na idara mbili ndogo za masoko na Habari.

Tumeona hizi ni idara mbili zinazofanana hivyo tumeamua kuunda moja ambayo tunataka kuitanua. Wambura atasaidiwa na mkuu wa masoko Aaron Nyanda na upande wa habari atakuwa akisaidiwa na Clifford Ndimbo.

Kamati ya ligi iliyokutana hivi karibuni imeagizwa kumtafuta mrithi sahihi wa Wambura. Wambura amekuwa akisimamia kanuni za mpira wa miguu na amekuwa akitoa adhabu kwa wachezaji ,makocha na hata viongozi pasipo kujali ukongwe na ukubwa wa vilabu hivyo.

Post a Comment

0 Comments