Unaambiwa gumzo kubwa ndani ya Simba hivi sasa ni kiwango alichokionesha kipa Beno Kakolanya katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Bandari FC.
Mechi hiyo iliyopigwa Jumamosi iliyo iliyopita katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ilimalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililowekwa kimiani na Ibrahim Ajibu baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa Rashid Juma dakika ya 77.
Licha ya Simba kushinda mechi hiyo, Kakolanya alikuwa shujaa baada ya kuokoa hatari kadhaa kutoka kwa mshambuliaji Mganda, Wadri William aliyepiga mashuti takribani matatu ambayo Kakolanya alienda nayo hewani.
Kakolanya alipangua mashuti ya William ambaye alikuwa na moto wa aina yake katika mchezo huo.
Kutokana na kazi ya Kakolanya, wadau na mashabiki wengi wa Simba walimsifia kipa huyo licha ya kutopata namba mbele ya Aishi Manula.
Wengi walimsifia haswa katika mitandao huku wakishauri ni vema apewe pia nafas ya kucheza kutokana na alivyofanya kazi nzuri.
0 Comments