BETI NASI UTAJIRIKE

KAGERE KUTIMKIA MAREKANI SIMBA KULAMBA MABILIONI

 Meddie Kagere anazidi kung'ara baada ya kupata dili jingine kutoka Marekani.Kagere mwenye mkataba na Simba mpaka mwaka 2021 anaweza kuondoka msimbazi kabla ya mwaka huo.




Taarifa kwa mujibu wa Meneja wa Kagere, Patrick Gakumba, ameibuka na kusema kwa kasi aliyonayo, tayari ameshamuandalia ofa nzuri katika klabu ya Dallas FC iliyopo Texas, Marekani.

Gakumba ameibuka na kusema moja kati ya masharti ambayo Dallas wanayataka ili Kagere wamchukue ni kuhakikisha anafikisha mabao 25 msimu huu kunako Ligi Kuu Bara,

“Najua kwa sasa Kagere ni mali ya Simba, nawasiliana naye nikimtaka azidi kuitumikia klabu hiyo kwa nguvu zote huku akikumbuka deni la mabao 25 linalohitajika.

"Dau la kule litakuwa ni nono zaidi ya Msimbazi, na tayari jina lake limeshajulikana katika nchi nyingi za Afrika na duniani kwa ujumla."

Mpaka sasa Kagere aliyecheza mechi nne msimu huu ameingia kambani mra sita huku wachezaji wanaofuatia ni Miraji Athumani na David Molinga walio na mabao matatu kila mmoja.

Post a Comment

0 Comments