Straika hatari wa Simba, Meddie Kagere, amefunga jumla ya mabao saba katika mechi tano alizocheza msimu huu katika Ligi Kuu Bara. huku Yanga wakifunga mabao 5 tu
kwenye mechi 4 walizocheza. Kagere alikuwa ana mabao sita na aliweza kuongeza la saba kufuatia kufunga tena dhidi ya Azam Fc .
Bao lake la saba linamfanya Kagere kuwazidi idadi ya mabao Yanga ambao ni watani zake wa jadi walio na matano pekee.
Kagere amefanikiwa kuwazidi Yanga kwa mabao mawili zaidi na kufanya azidi kukimbiza katika kuwania kiatu cha ufungaji bora msimu huu.
Kagere ataiongoza tena Simba siku ya tarehe 27 Oktoba dhidi ya Singida United mchezo utakaopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
0 Comments