advertise with us

ADVERTISE HERE

JINSI ZAHERA ALIVYONUSURIKA KUTIMULIWA YANGA

Kocha wa klabu ya Yanga  Mwinyi Zahera amejihakikisha uwepo wake kwenye kikosi hicho cha mabingwa wa kihistoria.

Msimu huu Zahera aliuanza vibaya zaidi baada ya kushinda mchezo mmoja kati ya michezo 6 ya michuano mbali mbali ikiwemo ligi kuu bara na ligi ya mabingwa Ulaya.

Kwa upande wa ligi ya mabingwa ulaya timu hiyo ilicheza michezo minne na kushinda mchezo mmoja kisha kudroo michezo miwili na kupoteza mchezo muhimu dhidi ya Zesco United ambao ungeipereka timu hiyo hatua ya makundi ligi ya mabingwa Africa.

Kwa Upande wa ligi timu hiyo imecheza michezo 3 huku ikipoteza 1 ,droo 1 na kushinda 1. Uwepo wa makame dhidi ya Coastal Union ulimfanya kocha huyo aendelee kuwepo.

Nini kilichopo nyuma ya pazia

Msimu uliopita klabu hiyo iligubikwa na migogoro mbalimbali na kupelekea baadhi ya wachezaji kutolipwa stahiki zao kwa wakati. Hilo lilipelekea baadhi ya wachezaji kucheza chini ya kiwango huku wengine wakiiacha klabu hiyo.

Mwishoni mwa msimu timu hiyo ilifanikiwa kumaliza nafasi ya pili na kufanikiwa kuingia ligi ya mabingwa Afrika.

Kocha Mwinyi Zahera alitumia mbinu mbalimbali kuwajenga wachezaji kisaikolojia na wakafanya vizuri ,kuna wakati aliwalipia wachezaji hao nauli za ndege na hotel ili tu kuwapa morali.

Kinachoendelea kwa Mashabiki wa Yanga.

Msimu wa 2019/2020 ulipoanza Yanga walipoteza mchezo dhidi ya Ruvu shooting, Mchezo uliofuata timu hiyo ilipata sare ya mabao 3-3 dhidi ya Polisi Tanzania huku Nchimbi akipiga hat trick ya kwanza. Baada ya mechi kumalizika mashabiki wa timu hiyo walianza kulalama Zahera aondoke kwani ameishiwa mbinu za ufundishaji.

Uongozi unasemaje kuhusu Zahera

Uongozi wa Klabu hiyo hauna matatizo yoyote na kocha huyo na wanaamini ni msaada mkubwa msimu huu jambo ambalo ni kweli kabisa . Lilipofunguliwa dirisha la usajili klabu hiyo ilipoteza nyota wake wanne kwenye kikosi cha kwanza akiwemo Makambo, Ajibu, Kakolanya hivyo kudhoofisha timu hiyo.

Mbali na hayo Zahera amekuwa ni mshauri wa mambo mbalimbali ndani ya Yanga hasa kuendesha klabu kwa faida kwani anakaa soka la kulipwa kwa muda mrefu

Post a Comment

0 Comments