BETI NASI UTAJIRIKE

HUYU HAPA KOCHA MPYA WA TAIFA STAZI ALIYECHUKUA NAFASI YA AMUNIKE

Baada ya sintofahamu iliyozuka hivi karibuni kuhusiana na nani atakuwa kocha wa kudumu wa timu ya Tanzania "Taifa Stars", hatimaye TFF wamemaliza kiu cha watanzania



TFF imemteua Etienne Ndayiragije kuwa Kocha Mkuu waTimu ya Taifa (Taifa Stars) kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Ndayiragije ambaye hivi karibuni amevunja mkataba na Azam FC, alikuwa kocha wa muda wa Taifa Stars tangu kuondoka kwa Mnigeria Emmanuel Amunike baada ya timu hiyo kufanya vibaya kwenye michuano ya AFCON 2019 nchini Misri.



Taarifa iliyotolewa hivi punde na TFF imeeleza kuwa uamuzi huo umezingatia mapendekezo ya kamati yake ya ufundi ambayo ilipitia wasifu wa makocha mbalimbali walioomba nafasi hiyo.


Maoni ya wadau

Wachambuzi mahili na wadau wa soka wameikosoa TFF kwa kufanya mambo kijanjajanja kwani kumpa Otieno mkataba wa mwaka mmoja ni kama kutokuwa na mipango endelevu kwa timu hiyo. Chini ya Otieno taifa stars imefanikiwa kuingia hatua ya makundi CHAN 2020 , Kuendelea na mchujo hatua ya makundi kufuzu kombe la dunia Qatar mwaka 2022. 

Post a Comment

0 Comments