advertise with us

ADVERTISE HERE

HUYU HAPA KOCHA ATAKAYECHUKUA NAFASI YA OLE GUNNAR MANCHESTER UNITED

Klabu ya Manchester United imeanza kupata wakati mgumu baada ya mashabiki kutaka Kocha wa sasa kuondolewa.Ole gunnar amejikuta katika wakati mgumu baada ya timu hiyo kushinda Michezo miwili tu kati ya nane iliyocheza ligi kuu Uingereza.

Mashabiki walianza kumtupia lawama Kocha huyo na kumtaka aondoke klabuni hapo ingawa uongozi wa timu hiyo umeendelea kuwa upande wake.

Nani wa kuchukua nafasi ya Ole gunnar?

Taarifa zisizo rasmi zimesema kocha Alex fergusson amependekeza jina la kocha wa zamani wa Juventus na Ac Milan  Massimilano Allegrili.

Kocha huyo mwenye miaka 52 amefundisha vilabu 7 tofauti huku akiiongoza juventus kutwaa mataji matano mfululizo ya Serie A,kuingia fainali mbili za UEFA ingawa zote alipoteza kwa timu za hispania Barcelona na Real Madrid.

Kocha huyo aliyemaliza miaka mitano ya kuifundisha Juventus nafasi yake ilichukuliwa na Maurio Sari.

Je atafit kuifundisha Manchester United?

Mashabiki wanaamini atafanya vizuri baada ya kuonyesha uwezo mkubwa akiwa na Juventus akitwaa mataji mengi na kufika hatua ya nusu fainali mara 4 mfululizo na fainali 2 .


Post a Comment

0 Comments