advertise with us

ADVERTISE HERE

HIVI MKAPA ALIKUWA SIMBA AU YANGA?

Na Maggid Mjengwa .

Nina bahati utotoni kushuhudia pale National Stadium siku Simba walipocheza na Vita ya Zaire.
Nakumbuka nilimkubali sana beki namba mbili wa Simba.


 Daud Salum, ni kwa jinsi alivyomkaba winga machachari wa AS Vita, Mayanga Maku. Tangu siku hiyo Daudi Salum akajipatia jina la ‘ Bruce Lee!’
Na yule Mayanga Maku kwa mujibu wa stori nilizosikia enzi hizo pale Ilala kwenye kijiwe cha kahawa kona ya mitaa ya Dodoma na Lindi, eti, watu wazima wale walisema jina la pili la Mayanga Maku lilikuwa gumu
Kutamkwa kama lingetamkwa kama ilivyopaswa!
Turudi kwenye swali la msingi; Mkapa Simba au Yanga?
Inasemwa, katika utawala wake, Benjamin Mkapa hakupata kuonekana kwenye viwanja vya soka. Ukweli hata mimi sijawahi kumwona Mkapa kwenye mechi ya mpira.
Ajabu ya Mkapa, wakati wananchi wake wakitafakari juu ya watafanyaje na uwanja wao wa taifa uliochakaa, ni Benjamin Mkapa aliyeahidi kuwajengea uwanja wa kisasa kabla hajamaliza muda wake, na akatimiza ahadi yake hiyo.
Nchi yetu kwenye kandanda kimsingi imegawanyika kati ya Simba na Yanga. Na viongozi wetu pia. Kama tulivyokuwa hatujui kama Nyerere alikuwa Simba au Yanga ndivyo ilivyokuwa kwa Mkapa.
Akiwa Rais Mstaafu, mwaka 2008 Benjamin Mkapa aliongea kwenye Ubalozi wa Finland. Ikaandikwa,
" Mkapa atoa neno!"
Ni kwenye moja ya magazeti yetu. Hilo " neno alilotoa" mara ya mwisho kuhusu kandanda ni wakati alipowaaga pale Ubalozi wa Finland, watoto wa kutoka kwao Mtwara waliokuwa safarini kwenda Finland kucheza soka.
Kuongea kule kwa Mkapa kulikuwa na tofauti kubwa. Ikaripotiwa, kuwa Mkapa kaongea kuhusu michezo.
Habari ikawa kubwa na maswali mitaani yakaendelea kuulizwa, na swali kuu lilikuwa;
" Jamani hivi Mkapa Simba au Yanga?
Waliokuwepo pale Ubalozini kuna waliomsikia Mkapa akitamka kupenda alama ya Simba katika michezo. Kuna mwandishi mwingine aliyeandika kuwa ni kweli Mkapa aliulizwa swali na mmoja wa watoto hao kuwa anapenda timu gani.
Mwandishi huyo akaandika, kuwa Mkapa alimjibu mtoto huyo
" Wee, acha utundu!"
Swali linabaki; Mkapa Yanga au Simba?

Post a Comment

0 Comments