Chama cha Soka nchini uhispania kimetangaza mabadiliko ya ratiba ya mechi baina ya Barcelona na Real Madrid.
Hilo limekuja hii leo baada ya kuwepo maandamano jijini Catalunya ambako ni makao makuu ya Barcelona na ambapo mchezo huo ulipangwa kupigwa tarehe 26-10-2019.
Taarifa iliyo rasmi inasema chama cha soka hispania Royal Spanish Footbal Federation (RFEF) limekili kupokea barua kutoka bodi ya ligi LA LIGA kuhusu kuhamishwa kwa mchezo huo.
Taarifa hiyo inasema Chama hicho kimekwisha fanya mazungumzo na klabu zote mbili na zimepewa muda mpaka siu ya jumatatu kutoa taarifa ya maombi yaliyotumwa, baada ya hapo majibu kurudishwa kaati itakaa na kutoa majibu yaliyo sahihi.
Taarifa sahihi itatolewa na chama hicho siku ya jumatatu kama mchezo huo utacheza Santiago Bernabeu badala ya Nou Camp.
0 Comments