advertise with us

ADVERTISE HERE

DI MARIA AELEZA ALIVYOLIZWA NA LIONEL MESSI

Mchezaji wa PSG na timu ya taifa Argentina hivi karibuni alifanya mahojiano na kituo cha televisheni ESPN.

Di maria ametoa siri ya Lionel Messi kuwaliza wachezaji wa Argentina mara baada ya kuondolewa michuano ya Copa America na wapinzani wao wakubwa Brazil hatua ya nusu fainali.

Argentina ilifungwa mabao 2-0 na Brazil huku Messi akiwa Kapteni wa kikosi hicho. Mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu ulipigwa dhidi ya Chile na Argentina kushinda mchezo huo. Di Maria alimnukuu Messi akisema "Nina furaha na timu hii nzuri tulioijenga, si wote tumekuwa tukiitwa kwenye hii timu mara kwa mara lakini tunaonekana kama tumekuwa pamoja kwa muda mrefu lakini pia tumeitumikia jezi yetu vile tuwezavyo, si kwamba hatukustahiri ila wenzetu walituzidi mbinu" Baada ya maneno hayo kila mmoja alitokwa na machozi chumbani humo.

Messi amekuwa akibeba lawama hasa timu yake Argentina inapofanya vibaya  tofauti na Barcelona na ameshutumiwa mara nyingi kutokuwa na mapenzi na Nchi yake.

Di Maria ameongeza kuwa "watu walimlaumu messi kutoimba wimbo waTaifa  tuhuma ambazo si kweli na Messi hakuwahi ziongelea. Copa America  hii Messi ameonekana tofauti ameonyesha uwezo mkubwa,ameongea na wanahabari pia ameongea na wachezaji wenzake vizuri,

Post a Comment

0 Comments