Ofisa Mtendaji mpya wa klabu ya Simba, Senzo Mazingisa ameonekana kuskitishwa na mwenendo mbovu wa timu hiyo kimataifa
kutokana na kuondolewa kunako Ligi ya Mabingwa Afrika mapema kabisa, imeelezwa.
Simba iliondolewa na UD Songo ya Msumbiji baada ya mechi ya raundi ya pili jijini Dar es Salaam kumalizika kwa sare ya 1-1.
Taarifa imeeleza kuwa kuondolewa kwa Simba kumemuumiza zaidi Mazingisa ambaye hivi karibu alisema wamemua kufanya marekebisho ili kutojirudia kwa makosa hayo siku za mbeleni.
Bosi huyo alieleza kuondolewa mapema kunako Ligi ya Mabingwa Afrika kumesababisha kwa namna moja ama nyingine kushindwa kutangaza jina la klabu vizuri.
Aidha, Mazingisa alieleza kwa sasa wapo kwenye mikakati kambambe ya kuhakikisha baadhi ya mabadiliko yanafanywa ili kuboresha mianya iliyo dhaifu mambo yaweze kwenda sawia kama wanavyotarajia.
0 Comments