Klabu ya Yanga imethibitisha kurejea kwa beki wake mahiri Paul Godfrey ambaye alikuwa majeruhi. Yanga imekuwa ikipata wakati mgumu baada ya beki huyo kukosekana mechi kadhaa za kimataifa.
Daktari Shecky magazija wa timu hiyo amethibitisha kurejea kwa beki huyo na ameshaanza mazoezi binafsi kabla ya kujiunga na kikosi cha kwanza. Daktari huyo amenukuliwa akisema "Boxer alipata majeraha upande wa goti la kulia na matibabu yake yalichukua muda kidogo ila tunashukuru Mungu kwa kuwa amepona ila amebakiwa na programu yake peke yake ili kujiweka fiti ,baada ya siku mbili atajumuika na wenzake na baada ya mechi na mbao ataungana na wenzake kikosini"
Yanga inajiandaa na mchezo dhidi ya mbao na ule wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Pyramids ya nchini Misri tarehe 27-10-2019 mchezo utakaopigwa jijini mwanza uwanja wa CCM KIRUMBA .
0 Comments