advertise with us

ADVERTISE HERE

ARSENAL ,LIVERPOOL NA CHELSEA ZAZIDI KUWAKA MOTO HUKU MANCHESTER CITY ,UNITED ZIKIPOTEANA

Klabu za Arsenal ,Chelsea na Liverpool zimeendelea kufanya vizuri zikiwa ugenini na nyumbani ligi kuu nchini Uingereza. Tukianza na Liverpool.

Liverpool iliwakaribisha nyumbani Leicester na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1. Maba ya Liverpool yaliwekwa kimiani na Sadio Mane dakika ya 40 na JAmes milner dakika ya 90+5  huku lile la Leicester likifungwa na James Maddison dakika ya 80

Matokeo hayo yanaifanya Liverpool kuongoza ligi  kwa tofauti ya pointi 8 dhidi ya Manchester City.

2.ARSENAL

Klabu ya Arsenal imeamka kutoka usingizini baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bournemouth goli pekee lililofungwa na David Luiz dakika ya 9. Kwa matokeo hayo Arsenal inashika nafasi ya 3 nyuma ya Manchester City kwa togauti ya pointi 1.3. CHELSEA 

Klabu ya Chelsea nayo imeamka usingizini baada ya kujipatia usindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya  Sanderland huku mabao hayo yakifungwa na Tammy Abraham dakika ya 7,Mason Mount 24, Kante 40 na Batshuayi 89. Kwa matokeo hayo Chelsea inasogea nafasi ya 5 nyuma ya Leicester City kwa tofauti ya magoli huku zote zikiwa na pointi 14.


4. TOTTENHAM 

Klabu hii yenye maskani yake pale White Hart Lane imeendelea kupata tabu wiki hii baada ya kupigwa mabao 3-0 dhidi ya Brighton Holvers. Kwenye mchezo huo dakika ya 3 na Maupay huku Connoly akishindilia msumari mzito wa mabao mawili dakika ya 32 na 65. Matokeo hayo yanaipeleka Tot nafasi ya 9 ikiwa na pointi 11.


5. MANCHESTER CITY 

Manchester city imeendelea kuwa na wakati wa kushangaza baada ya kushinda mechi moja kati ya tatu ilizocheza kweny ligi . Baada ya kupigwa mabao 2-0 dhidi ya Wolves imejikuta ikisalia pili kwa tofauti ya pointi 9 dhidi ya Liverpool inayoongoza Ligi.


6. MANCHESTER UNITED

Klabu hii imeendelea kuwa na msimu mbaya zaidi baada ya kufungwa na klabu ya Newcastle United bao 1-0 imetupwa nafasi ya 12 na kuzua sintofahamu ndani ya timu hiyo.

Post a Comment

0 Comments