TFF imemfungia beki wa Kagera Sugar kucheza mechi mbili kwa kosa la makusudi akitaka kumvunja kiungo mshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajibu.
tukio hilo lilitokea wakati Simba ikocheza na Kagera Sugar mchezo wa ligi kuu Vodacom msimu wa 2019/2020.
Mwamuzi wa mechi hiyo alimpa kadi ya njano mchezaji Zawadi na alistahiri kupewa kadi nyekundu.
mara baada ya mechi hiyo mchezaji huyo alimuomba radhi Ajibu kupitia mitandao ya kijamii na kukuri kosa lake.
TFF kupitia mjumbe wake kamati ya maadili amesema waliipitia kwa umakin video ya mechi hiyo na kuamua kumfungia Zawadi michezo miwili huku Mwamuzi wa mechi hiyo akionywa vikali
0 Comments