advertise with us

ADVERTISE HERE

ALICHOSEMA MSEMAJI WA YANGA KUELEKEA MECHI NA JKT TANZANIA

Mabingwa wa Kihistoria ligi kuu Tanzania bara leo hii wataingia uwanjani kuwakabili JKT Tanzania kwenye mchezo wa ligi kuu Vodacom. Habari ni njema kwa timu hiyo kongwe kwani baadhi ya wachezaji wake watareje uwanjani.

Mshambuliaji mpya wa timu hiyo Moringa ataingia uwanjani kwa mara ya kwanza na anategemewa kufanya mambo makubwa . Mhamasishaji wa Yanga BwanaAntonio Nugaz amesema Yanga itakwenda uwanjani na kauli mbiu isemayo " MORINGA IS BACK".

Mshambuliaji huyo hakushiriki michezo minne ya Ligi ya Mabingwa Afrika kutokana na kukosa vibali maalumu kutoka CAF.

Mbali na Molinga kurudi uwanjani mchezaji mwingine ni Bigirima ambae alikuwa majeruhi tangu ligi asajiliwe na sasa amerejea rasmi baada ya mguu wake kukaa sawa.

Balama alieumia kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Africa dhidi ya Zesco jijini Dar es salaam atarejea dimbani kuwakabili JKT Tanzania.

Hapo jana Yanga ilifanya mkutano na wanahabari na msemaji wa timu hiyo Antonio Nugaz alinukuliwa akisema

"Unapocheza na Yanga mechi za kirafiki ni tofauti na mashindanoni, mchezo na JKT utakuwa mgumu lakini sisi tunakwenda kuianza ligi rasmi baada ya mechi ya awali dhidi ya Ruvu Shooting kupoteza, kwahiyo mategemeo yetu ni hizi mechi mbili zijazo tutasogea pointi sita ili tuweze kurejea kwenye nafasi yetu tunayostahili ya kuongoza ligi hapo baadae na kutwaa kombe"

Post a Comment

0 Comments