advertise with us

ADVERTISE HERE

ZESCO WAIHUJUMU YANGA KABLA YA MECHI

Leo jioni Yanga itaumana na Zesco United kwenye mchezo wa pili wa ligi ya Mabingwa Africa na dhahiri Zesco wanaiogopa Yanga.


Mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar Es Salaam ulimalizika kwa timu hizo kufungana bao 1-1 na Zesco waliondoka jijini Dar es Salaam bila kupata changamoto yoyote.

Mchezo wa pili unapigwa leo mjini ndola na Zesco walianza figisu tangu siku ya kwanza timu hiyo ilipokuwa inawasili.

tangu mabosi Yanga watue katika mji wa Ndola, Zambia wamekuwa wakikatiwa umeme mara kwa mara, jambo ambalo limesababisha mawasiliano kuwa magumu.

Mabosi hao wapo Ndola tangu Jumapili iliyopita kwa ajili kufanya maandalizi ya mechi dhidi ya Zesco ambayo ni ya raundi ya pili ya ligi ya Mabingwa Afrika itakayofanyika leo kwenye uwanja wa Levy Mwanawasa.

Mbali na umeme pia kumeuwa na shida ya mtandao ambao umesababisha kusiwe na mawasiliano mazuri baina yao kama viongozi na hata wachezaji.

Kaimu Mwenyekiti wa Yanga amekiri uwepo wa tatizo hilo kuwa limesababisha changamoto kwao kama viongozi.

"Tangu tumefika hapa kumekuwa hakuna huduma nzuri ya umeme maeneo mengi, hata hotelini tulipofikia kwani unapatikana kwa saa chache na ndiyo sababu unaona muda mwingine sipo hewani", alisema Msolla.

Post a Comment

0 Comments