BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA WAIGOMEA TFF NA MDHAMINI WA LIGI

Uongozi wa klabu ya Yanga umepeleka malalamiko kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ukipinga uamuzi wa Bodi ya Ligi kumfungia kocha wake Mwinyi Zahera mechi tatu kutokana na shutuma alizotoa kwa bodi hiyo baada ya mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting.




Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela (Pichani: Kushoto) amesema adhabu ya kumfungia kocha mechi tatu ni kubwa na kushauri kuwa ni bora angepigwa faini hivyo hawaoni kama bodi hiyo imetenda haki.
"Unapomfungia kocha mechi tatu kwa nini usimpe faini tu aendelee kufundisha timu?," amehoji Mwakalebela na kusema "Tumeshaiandika barua wizara … tunasubiri majibu"
Katika mchezo huo wa Ligi Kuu kocha Zahera alilalamikia hatua ya Bodi ya Ligi kukataa kusogeza mbele kwa siku mbili mechi dhidi ya Ruvu Shooting ili wapate muda wa kupumzika na kufanya maandalizi.

Yanga imefikia maamuzi hayo baada ya kufungwa na timu ya Ruvu shooting bao 1-0. Mbali na hayo klabu hioyo imemgomea mdhamini wa ligi hiyo (vodacom) kwa kusema haina utamaduni wa kuvaa rangi nyekundu na hivyo haiporadhi kupokea jezi yoyote yenye nembo nyekundu.

Post a Comment

0 Comments