advertise with us

ADVERTISE HERE

YANGA KUIBOMOA ZESCO BILA MOLINGA NA MUSTAFA

Klabu ya Yanga SC leo itaingia uwanjani kumenyana na Zesco United ya Zambia kwenye mchezo wa ligi ya Mabingwa Afrika. Mchezo huo utapigwa jijini Dar es Salaam na mchezo wa pili utapigwa tarehe 27/9 huko Lusaka Zambia.

Msemaji wa klabu hiyo bwana Dismas ametoa ufafanuzi kwamba Molinga na Mustafa watakosa mchezo huo baada ya vibali vyao kuchelewa kutoka CAF.
Bwana Dismas amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa na kuishangilia klabu hiyo kwana maandalizi waliyoyafanya jijini mwanza yanatosha kabisa kuiangamiza Zesco.

Kocha wa Zesco Bw.Lwandamira  anaonekana si tishio kwa klabu ya Yanga mbali na kwamba aliiongoza klabu hiyo kabla ya Mwinyi Zahera na anawafahamu nusu ya wachezaji wa Yanga lakini yanga wamesisitiza wanamheshimu na hawezi wadhalilisha.
Mbali na hayo inasemekana Lwandamina anawadai Yanga baadhi ya fedha ambazo walishindwa kumlipa kabla ya kutimkia zesco.

Post a Comment

0 Comments