Klabu ya Yanga imetangaza vita vikali dhidi ya Zesco United. Yanga imeweka kambi jijini mwanza kujiandaa na mchezo huo wa ligi ya mabingwa Afrika.
Yanga ni timu pekee kutoka Tanzania iliyopenya kwenye raundi ya kwanza kwenye michuano hiyo ya CAF ikiing'oa Town Rollers ya Botswana kwa jumla ya mabao 2-1 na sasa itavaana na Zesco Unoited kutoka nchini Zambia. Mechi ya kwanza itapigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na mchezo wa marudiano utafanyika nchini Zambia.
Kma Yanga itashinda mechi hiyo basi itafuzu moja kwa moja kwenye hatua ya makundi ya michuano hiyo. Kila la kheri kwa klabu ya Yanga.
0 Comments