advertise with us

ADVERTISE HERE

WACHEZAJI STAZI WALETA MGOMO MWINGINE DHIDI YA BURUNDI

Unakumbuka ule mgomo wa Taifa Stazi kule Misri. Basi Stazi imerudia yaleyale kwa staili nyingine 

Wakati wa mapumziko wachezaji wa kikosi cha Taifa Stars juzi waligoma kuingia vyumbani ili kuwavuruga kisaikolojia wenyeji katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia Qatar 2022 dhidi ya Burundi.

Stars waligoma kuingia vyumbani baada ya kuhisi harufu za ajabu ambazo walikuwa hawazielewi, hivyo viongozi wakashauri wabaki nje.

Katika mzozo huo, Watanzania watatu, walikamatwa na wanajeshi wa Burundi na kuwekwa kizuizini hadi tunakwenda mitamboni walikuwa hawajaachiwa.

Kikosi cha Stars: Juma Kaseja, Haruna Shamte, Gadiel Michael, Kelvin Yondani, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Sure Boy, Himid Mao, Samatta, Msuva na Hassan Dilunga.

Post a Comment

0 Comments