advertise with us

ADVERTISE HERE

STRAIKA YANGA KULIPWA MIL 2 KWA KILA BAO


Kocha Mkuu wa Yanga, Mkongomani Mwinyi Zahera ametenga kitita cha milioni mbili kwa ajili ya kununua mabao ya straika wake David Molinga ‘Falcao’ raia wa DR Congo katika Ligi Kuu Bara.


Zahera ametenga kitita hicho ikiwa  ni baada ya straika wake huyo kuanza  kuonyesha cheche kwa kufunga  mabao matatu kwenye mechi zao  mbili zilizopita za kirafiki.

Molinga alifunga  mabao hayo  kwenye mechi za  timu hiyo dhidi  ya Pamba SC  na Toto  African  wakati  walipokuwa  Mwanza  wiki chache  zilizopita.

Zahera amesema  kwamba atatoa kiasi hicho cha milioni 2,293,230 (sawa na dola 1,000)  endapo kama itatokea straika wake  huyo atashindwa kufunga mabao 15  au zaidi kwenye ligi kuu. “Mimi ninasema nitatoa kiasi cha  dola 1,000 kama itatokea Molinga  hatafunga mabao 15 kwenye ligi kuu.

Ninamjua ana uwezo mkubwa wa  kufunga tofauti na watu ambavyo  wanamchukulia,” alisema Zahera  ambaye ameuweka kando uraia wa  DR Congo na kuchukua wa Ufaransa.

“Hapa kwenye kikosi changu tatizo  lililopo ni washambuliaji tu kushindwa  kufunga mabao. Sisi kwenye mechi  moja tunaweza kupata hadi nafasi sita  lakini tukafunga mabao machache  huku nyingi tukikosa.

“Yaani hatuna shida kabisa kwenye  kutengeneza pasi za mabao ila tatizo  ni kufunga lakini muda si mrefu  nitatengeneza mbinu ambayo itafanya  tufunge katika kila nafasi ambayo  tunaipata,” alisema Zahera ambaye ana mtihani mkubwa wa kuivusha  Yanga kimataifa ili kurejesha imani ya  kikosi chake kwa mashabiki

Post a Comment

0 Comments