advertise with us

ADVERTISE HERE

SIMBA YAMTAMBULISHA CEO WAKE MPYA

Simba SC imemtambulisha rasmi Senzo Mazingiza kutoka nchini Afrika Kusini kuwa Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) mpya wa klabu hiyo, akichukua nafasi ya Crescentius Magori anayemaliza muda wake.
Akizungumza wakati wa utambulisho huo uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam, Senzo ameahidi kuifanya Simba kuwa timu kubwa zaidi barani Afrika.

"Simba ni timu kubwa sana, nimekuwa naifuatilia kwa muda sasa. Nimejifunza kuwa ni timu kubwa, na tunaweza kuifanya kuwa kubwa zaidi, siyo tu ukanda wa Afrika Mashariki bali kuwa klabu kubwa zaidi Afrika," kauli ya Senzo Mazingiza.
Naye CEO anayemaliza muda wake Crescentius Magori amewashukuru Wanasimba kwa ushirikiano waliompa kwa kipindi cha takriban miezi minane ambayo amekamata nafasi hiyo.
"Kuanzia wiki ijayo nitakuwa CEO mstaafu. Nawashukuru sana kwa ushirikiano mlionipa. Nawashukuru sana Wanasimba. Kwa tuliokwazana niwaombe radhi ilikuwa sababu ya kazi yangu”, amesema Magori.

Post a Comment

0 Comments