advertise with us

ADVERTISE HERE

SIMBA WAIKOMESHA YANGA DHIDI YA ZESCO

Unakumbuka ule usemi usemao "Zesco njooni mashabiki mtapata hapa hapa" hilo linadhihirika leo baada ya jezi za Zesco kuonekana dili jijini Dar es salaam.
Mashabiki wa Simba wametangaza kuishabikia Zesco na wananunuia jezi hizo zilizomwagika kama utitili jijini Dar es salaam.

Zesco United itavaana na Yanga katika dimba la mkapa jijini Dar es salaam na mchezo utakaofuata utapigwa jijini Lusaka nchini Zambia.

Msem,aji wa Simba SC amemwagia petroli kwenye moto na kusisitiza kuishangilia klabu ya Zesco dhidi ya wapinzani wao wa jadi Yanga.

kupitia ukurasa wake wa instagram manara aliweka picha na kuandika "Mida ya jioni jioni hyo kesho,,
Hapo mtu keshakula thalatha safi kabisa ,,Kama nawaona mbute mbute"

Picha kutoka maktaba , haihusiani na mchezo wa leo dhidi ya Zesco.

Post a Comment

0 Comments