Mchezaji mkongwe wa Cameroon Samuel Eto'o Amethibitisha Kustaafu Soka Akiwa na Umri wa Miaka 38. Hii ni huzuni kwa wapenzi wa soka hasa bara la Africa.
Eto'o alianza Safari yake ya Soka Barani Ulaya Mwaka 1996 akitua Real Madrid, Baada ya Miaka 23 katika Soka kuvitumikia . Eto'o ameshinda makombe mbalimbali ikiwemo UEFA champions League akiwa na Barcelona pamoja na Intermilan na amefunga magoli jumla ya magoli 350 katika Vilabu 13 tofauti ndani ya Mataifa Sita tofauti. Eto'o anastaafu Soka Akiwa Nchini Qatar katika Klabu ya Qatar SC.
Hivi karibuni Etoo alifanya mazungumzo na Canal+ na kuweka wazi nia yake ni kuja kuwa kocha hapo baadae na kufundisha moja ya vilabu barani Ulaya.
Eto'o anatajwa kama mchezaji mwenye heshima zaidi kwa Cameroon na Afrika kwa ujumla. Ameipa kcameroon kombe la mataifa ya Afrika mara mbili na kuisaidia timu hiyo kufika robo fainali kombe la dunia. Eto'o ametwaa tuzo ya mchezaji bora Afrika mara nne na kumfanya awe ni mmoja wa wachezaji wakubwa zaidi Africa.
.
0 Comments