advertise with us

ADVERTISE HERE

RONALDO ATWAA TUZO NYINGINE

Mshambuliaji wa Ureno na Juventus Cristiano Ronaldo amezidi kujiwekea historia baada ya kutwaa tuzo ya 10 kama mchezaji bora wa mwaka nchini Ureno. Hii ikiwa ya pili kunyakuwa katika siku za hivi karibuni baada ya ile ya Marca’s Legend award kutoka Hispania.


Ronaldo mwenye umri wa miaka 34, amekuwa akifanya vizuri kwenye tuzo hizo tangu mwaka 2007. Huku akiisaidia klabu yake ya Juventus kutwaa taji la nane mfululizo la Serie A.
Nyota huyo ametwaa tuzo hiyo kwa kumshinda kinda wa Atletico Madrid, Joao Felix, mchezaji wa Manchester City, Bernardo Silva, kiungo wa Sporting Lisbon, Bruno Fernandes na Ruben Neves  wa Wolves.Amekuwa akishinda tuzo hiyo mfululizo tangu 2007 waka mwaka 2010 na 2014 ndiyo kipindi pekee ambacho hakuchukua. Kwa sasa anaongoza akichukua mara 10 akifuatiwa na Luis Figo aliyechukua mara sita (6) pekee.

Tuzo hizo zimetolewa huko Carlos Lopes Pavilion katika jiji la Lisbon mahala ambapo Ronaldo amekulia wakati alivyokuwa kijana mdogo. Mchezaji huyo alipata nafasi ya kuzungumza mara baada ya kuchukua tuzo hiyo.
“Huu ulimwengu unakwenda kasi sana, watu wengi wamekuwa bize katika mitandao ya kijamii. Imekuwa ni mwaka mgumu sana kwa mtu mmoja mmoja, lakini usikubali mtu yoyote akukatisha tamaa. Sina msada lakini naweza kusema Sporting inastahili zawadi hata kidogo, muda ujao.” Cristiano Ronaldo
Washandi mbalimbali wa tuzo hizo za Ureno

Mchezaji bora wa mwaka wa kiume: Cristiano Ronaldo (Juventus)

Mchezaji bora wa mwaka wa kike : Jessica Silva (Levante / Lyon)

Kocha bora wa mwaka wa kiume : Bruno Lage (Benfica)

Kocha bora wa mwaka wa kike : Miguel Santos (Braga)

Timu bora kwa upande wa wamaume tuzo imekwenda kwa : Benfica

Timu bora kwa upande wa wanawake imekwenda kwa : Benfica


Post a Comment

0 Comments