Macho ya watanzania yalikuwa huko zimbabwe na Zambia wakifuatilia ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Zesco na Yanga pamoja na kombe la Shirikisho kati ya Triangle Vs Azam.
Hapa nyumbani ligi kuu Tanzania Bara iliendelea kama kawaida na kulichezwa michezo kadhaa jumamosi .
Mechi ya kwanza iliwakutanisha Mbao FC vs Mwadui FC na ilimalizika kwa sare ya bao 1-1, mchezp huo ulichezwa mkoani Shinyanga.
Alliance wameendeleza ubabe wao baada ya kuwafunga Singida United kwa bao1-0 mkoani Singida.
Klabu ya Ruvu shooting imeendeleza mpapaso baada ya kuipapasa Yanga mchezo wa kwanza wa ligi kuu ,imerudia tukio hilo kwa kuipapasa timu ya Polisi Tanzania kwa bao 1-0.
Aidha kocha mkuu wa timu hiyo bw.Salumu Mayanga alisema " Ulikuwa mchezo mgumu lakini tunashukuru kupata ushindi ugenini na inatuweka katika nafasi nzuri zaidi"
Ruvu shooting imepanda mpaka nafasi ya tatu ya ligi kuu ikiwa na jumla ya pointi 8 kwa michezo minne.
0 Comments