advertise with us

ADVERTISE HERE

MOURINHO ALAMBA DILI NONO,KUREJEA BARCELONA

Kocha mwenye mafanikio makubwa barani Ulaya Jose Mourinho amelamba dili jingine nono na mtandao wa livescore.com

Mara baada ya kutimuliwa kuinoa Manchester united, Mourinho alipata dili la kuwa mchambuzi wa kituo cha television BEIN SPORTS akishirikiana na kocha mstaafu wa Arsenal Arsene Wenger.

Mtandao wa livescore ambao hutoa matokeo ya moja kwa moja kutoka uwanjani umekuwa ukufanya vizuri na kwa sasa unashiRikiana na LA Liga kwa ajili ya matangazo mbalimbali. Mourinho amepata fursa hiyo kama moja ya mabalozi wa mtandao huo.

Hivi karibuni mtandao huo ulikuwa ukisherehekea ushirikiano na La Liga jijini Madrid na Mourinho alishiriki hafla hiyo pamoja na mastaa wengine kama Samuel Eto'o.

Mara baada ya sherehe hiyo ,Samwel Eto anasema" Nimechoka kudhihirisha kwamba Jose Mourinho ni mmoja ya watu wazuri katika soka ,nilipotangaza kustaafu alikuwa ni mtu wa kwanza kunipongeza. Mourinho anahitaji heshima na litakuwa jambo la heri kama atarejea Barcelona".
Mourinho na Eto'o wameshirikiana pamoja wakiwa Inter milan na walifanikiwa kutwaa ligi ya mabingwa ulaya.

Mourinho ameshirikiana na Eto'o wakiwa na Chelsea. Mourinho hupenda kumtumia kutokana na uwezo wake wakufunga pamoja na nguvu nyingi.

Mourinho amewahi kufanya kazi na klabu ya Barcelona kama mkalimani wa kocha aliestaafu Van Gaal ,hivyo Eto'o angetamani kumwona kocha huyo akiifundisha Barcelona

Post a Comment

0 Comments