BETI NASI UTAJIRIKE

MOURINHO ALALAMIKA ETO'O KUKOSA BALLON D'OR

Mkufunzi wa zamani wa Manchester United na Chelsea Jose Mourinho anaamini kwamba mchezaji wa miaka mingi Sameul Eto’o alistahili kutwaa tuzo Ballon d’Or walau moja.
Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona mwenye umri wa miaka 38 alistaafu hivi karibuni  katika mchezo wa soka.
Moja kati ya matokeo yake bora kabisa kwenye kipindi chake cha miaka 22 ambao ulihusisha kushinda kombe la bara Afrka mara mbili na kombe la mabingwa Ulaya mara tatu.
Mourinho kwa mara ya kwanza alifanya kazi na mchezaji huyo akiwa Inter Milan wakati wa msimu wa 2009/2010 ambapo wawili hao walishinda mataji matatu katika msimu mmoja likiwemo taji la Serie A, Kombe la Itali na kombe la mabingwa Ulaya.
Wawili hao kwa mara nyengine walifanya kazi pamoja katika klabu ya Chelsea miaka mitatu baadaye kwa muda mfupi.
”Ni vigumu kuelewa ni kwa nini Eto’o hakushinda taji la Ballon d’Or kufuatia kipindi chake cha soka” , alisema Mourinho katika mahojiano na Radio Cameroon.
”Samuel alichezea timu bora katika ligi bora duniani. Alifunga magoli mengi mazuri na alifanikiwa akiwa katika ligi tofauti”, aliongezea.
Alishiriki katika fainali tatu za ligi ya mabingwa Ulaya , akishinda mara mbili na Barcelona huku akifunga katika fainali zote mbili.
Pia alishinda kombe la mabingwa Ulaya mara moja akiichezea Inter mbali na kushinda mataji mengi ya ligi.
”Alikuwa mshambuliaji bora duniani kwa miaka kadhaa na nafikiria alihitaji kushinda taji la Ballon d’Or lakini haya ni mambo ambayo hatuna udhibiti nayo”.
Samuel Etoo alishinda mara nne taji la mchezaji bora wa Afrika huku tuzo bora ya fifa aliyopata ni ile ya kuwa katika nafasi ya tatu 2005.
Mbali na kushinda kombe la mataifa ya Afrika 2000 na 2002 aliibuka kama mfungaji magoli mengi akiwa na magoli 18.

Post a Comment

0 Comments