advertise with us

ADVERTISE HERE

MKUDE AWAZINGUA SIMBA,YANGA YATAJWA

Kiungo Mkabaji wa Simba, Jonas Mkude, Jumatano ya wiki hii alijiondoa kaambini na kuelekea kusikojulikana.
Taarifa za ndani zinaeleza Mkude aliamua kuondoka katika kambi ambayo Simba waliweka katika hoteli ya Sea Scape kabla ya kuelekea Kaegera kwa ajili ya mechi na Kagera Sugar.

Kiungo huyo hakuwa sehemu ya kikosi cha wachezaji Simba ambao walisafiri kuelekea Kagera japo ilielezwa Kocha Patrick Aussems alikuwa kwenye mipango ya kumtumia.

"Aliondoka hapa kambini usiku na haikujulikana ameleekea wapi sababu akitafutwa simu zake hazipatikani", kieleza chanzo.

Lakini baadaye Mkude mwenyewe alipopatikana kwa simu aliulizwa juu ya suala hilo alikanusha kwa kusema: "taarifa hizo si za kweli, mimi nipo,"

Alipotakiwa kufafanua kwa kina aligoma kuzungumza chochote kile.

Licha ya kugoma kuzungumza, tulipomtafuta Ofisa Mtendaji wa Simba, Senzo Mazingiza, yeye alisema: "Tunaelekeza nguvu zetu kwenye mechi ya ligi dhidi ya Kagera Sugar, la mkude hatuwezi kulizungumza kwa sasa."


Vyanzo makini vinadai Mkude amekuwa akiwindwa na Yanga tangu msimu uliopita na ameonyesha nia ya kujiunga na Mabingwa hao wa kihistoria .

Post a Comment

0 Comments